logo
MLIMANI SDA

Karibu!

Karibu katika kanisa la Waadventista Wasabato - Mlimani. Ibada zetu ni kila Sabato Jumamosi, Karibu ujiunge tushiriki wote kwa pamoja katika kujifunza neno la Bwana wetu Yesu Kristo. Wakaribishe ndugu, jamaa, rafiki na familia kwa ujumla.

Mathayo 11: 28-30 - "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi."

Kutuhusu

Kutuhusu

Karibu jimbo kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania. Sisi ni sehemu ya Kanisa la Waadventista wa sabato ambayo ni jamii ya watu waliokusudia kukuza uhusiano wa karibu kabisa na Mungu pamoja na kuwa na mwenendo kama aliokuwa nao Yesu. Kiini cha utume wetu ni kuushuhudia ulimwengu juu ya tumaini pekee lenye baraka linalotokana na uzoefu binafsi wa mahusiano bora na Mungu Mwokozi wetu mwenye Upendo, na kujiandaa kwa tukio kubwa kabisa la marejeo yake ambayo yamekaribia sana.

Kanisa la Waadventista wa sabato linajitambua kuwa kanisa la masalio la unabii wa Biblia wa siku za mwisho. Washiriki wa kanisa hili kwa pamoja huelewa jukumu lao maalumu kama mabalozi wa ufalme wa Mungu, na wajumbe wa marejeo ya Yesu Kristo yaliyo karibu. Waadventista wasabato wamejiandikisha kama jeshi la wafanyakazi pamoja na Mungu katika utume wa kuurejesha ulimwengu kutoka katika nguvu na uwepo wa uovu, kama sehemu ya pambano kuu baina ya Kristo na Shetani. Kwa hiyo, kila hali ya maisha ya mshiriki wa Kanisa huathiriwa na kusadiki na kuamini kuwa tunaishi katika siku za mwisho za unabii wa Biblia na kwamba kurudi kwa Yesu Kristo kuko karibu sana. Waadventista wasabato wameitwa na Mungu kuishi katika ulimwengu huu. Kila tendo la maisha ya Mkristo hufanyika “katika jina la Yesu” na kutangaza ufalme wake.

UTUME WA KANISA

Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato ni kuwafanya watu wote wawe wanafunzi wa Yesu, kutangaza injili ya milele katika Ujumbe wa maliaka wa tatu, Ufunuo 14:6-12, na kuuanda ulimwengu kwa marejeo ya Kristo yaliyo karibu.

UTEKELEZAJI WA UTUME WETU

Kwa kuongozwa na biblia na roho mtakatifu, waadventista wasabato hutekeleza utume huu kupitia maisha yanayoakisi alivyoishi Kristo, katika kuwasiliana, kufanya wanafunzi, kufundisha, kuponya na kuhudumia.

NJOZI YA UTUME WETU

Kwa kupatana na mafunuo ya Biblia, Waadventista wa Sabato tunauona utume wetu ukifikia kilele katika mpango wa Mungu wa urejeshwaji wa viumbe vyake katika ukamilifu wa mapenzi yake na haki yake.

Masomo Ya Sauti Ya Unabii

“Masomo ya Sauti ya Unabii” ni mpango wa kujifunza Biblia unaotolewa na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) kwa lengo la kuwasaidia watu kuelewa mafundisho ya Biblia kwa utaratibu na kwa kina. Masomo hayo huandaliwa kwa mfumo wa vitabu au maswali ya kujibu, yakihusisha mada mbalimbali kama wokovu, Yesu Kristo, unabii wa Biblia, Sabato, amri za Mungu, na maisha ya Kikristo. Programu hii hutumika kama njia ya uinjilisti na ukuaji wa kiroho, ambapo mwanafunzi hujifunza hatua kwa hatua na wakati mwingine hutunukiwa cheti baada ya kumaliza kozi.

Ratiba ya Ibada

Karibu tushirikiane katika vipindi vyetu mbalimbali vya ibada kila wiki.

Jumatano

Ibada ya Maombi

17:00 Hrs - 18:00 Hrs

Ijumaa

Kufungua Sabato

18:00 Hrs - 19:00 Hrs

Jumamosi

Ibada Kuu

09:00 Hrs - 18:00 Hrs

Viongozi

.

Jina: Abednego Masanja

Wadhifa: Mzee wa kanisa

Jina: Angallo Angallo

Wadhifa: Mzee wa kanisa

Jina: Omary Mbwambo

Wadhifa: Mzee wa kanisa

Jina: Steven Senjiro

Wadhifa: Mzee wa kanisa

Jina: Godfrey Machota

Wadhifa: Mzee wa kanisa