Muundo wa kanisa, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa kiroho wa washiriki na kwa ajili ya utekelezaji wa utume wa Kanisa. Muundo huo ni mhimili wa jumuiya ya kikanisa. “Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo” (Efe. 4:16).
Huduma Za Watoto
Huduma za watoto hukuza imani ya mtoto tangu kuzaliwa mpaka umri wa miaka 14; 0-3 Awali, 4-6 Chekechea, 7-9 Msingi, 10-12 Vijana wadogo.
zikiwaelekeza katika umoja na Kanisa. Hujaribu kutoa huduma mbalimbali zitakazowaelekeza watoto kwa Yesu na kuwafundisha kutembea naye kila siku. Hushirikiana na Shule ya Sabato na idara zingine kutoa elimu ya dini kwa watoto na hutimiza utume wake kwa kuanzisha huduma mbalimbali za watoto zenye mwelekeo wa neema zinazojumuisha watoto wote, zenye mwelekeo wa huduma, zinazojenga uwezo wa kuongoza, zilizo salama na za uinjilisti. “Mafunzo ya awali ya watoto yana umuhimu usiopimika. Mambo ambayo mtoto hujifunza katika miaka saba ya kwanza ya maisha yana mchango mkubwa zaidi katika kujenga tabia yake kuliko yote anayojifunza katika miaka inayofuata.”
Mawasiliano
Huduma ya mawasiliano inahitaji msaada wa kila mlei, kila mfanyakazi wa Kanisa na kila taasisi ya kanisa.
Idara ya mawasiliano huhamasisha utumiaji wa programu thabiti ya uhusiano na mbinu zote za kisasa za mawasiliano, tekinolojia endelevu na vyombo vya habari katika kueneza injili. Inalipasa kanisa kuchagua katibu wa mawasiliano na kamati ya mawasiliano kama inahitajika. “Inatupasa kutumia kila njia iliyo halali kuleta nuru kwa watu. Vyombo vya habari vitumike, na kila shirika la matangazo litakalovuta usikivu juu ya kazi ya Mungu.”
Elimu
Taasisi za kanisa huendesha shule kuanzia chekechea hadi chuo kikuu kwa makusudi ya kuwapatia wanafunzi kanuni za maisha,
Imani, mitazamo, maadili, tabia na desturi za Kanisa. Chanzo, mbinu na makusudi ya elimu ya Kiadventista ni elimu halisi ya Mungu, ushirika na uhusiano na Mungu katika masomo na huduma, na kufanana naye katika kujenga tabia.
Huduma Za Familia
Madhumuni ya huduma za familia ni kuimarisha ndoa na familia.
Familia ilianzishwa kwa uumbaji wa Mungu na ndoa ikiwa kiini chake. Kama mahali pa awali ambapo maadili hufundishwa na uwezo wa kuhusiana na Mungu na watu wengine hujengwa, ustawi wake ni muhimu kwa kazi ya Kanisa ya kufanya watu wawe wanafunzi.
Huduma za familia hudumisha fundisho la Biblia kuhusu familia na huinua kiwango cha maisha ya familia kilichowekwa na Mungu. Wakati huo huo, huleta huruma wakati wa huzuni inayowapata watu na familia katika ulimwengu ulioanguka. Idara hii hufanya kuwe na huruma, umoja, na upendo nyumbani na katika familia ya Mungu.
Huduma Za Afya
Kanisa linaamini kuwa wajibu wake wa kumfanya Kristo ajulikane ni pamoja na wajibu wa kimaadili wa kuhifadhi utu wa mtu kwa kuhimiza viwango vya juu vya afya ya kimwili, kiakili na kiroho.
Pamoja na kuwahudumia wanaougua, jukumu hili linakwenda mpaka kwenye uzuiaji wa magonjwa kwa kutumia elimu ya afya inayofaa na uongozi katika kuhimiza afya murua bila kutumia tumbaku, vileo, dawa zingine za kulevya na vyakula najisi. Inapowezekana, washiriki watahimizwa kimsingi kutokula vyakula vya nyama.
Huduma Za Uchapishaji
Huduma za uchapishaji huratibu na kukuza uinjilisti wa vitabu chini ya usimamizi wa baraza la huduma za uchapishaji pamoja na taasisi husika katika eneo hilo.
Husaidia idara zingine katika kutangaza, kuuza na kusambaza majarida yanayolipiwa kabla ya kuchapwa pamoja na machapisho mengine ya utume. Idara hii hufanya kazi na mchungaji na idara zingine katika kuandaa utaratibu wa kuwashirikisha washiriki katika huduma za uchapishaji. “Kuna mahali pengi ambako sauti ya mchungaji haiwezi kusikika, mahali ambako kunaweza kufikiwa na machapisho yetu tu—vitabu, magazeti, na vitini vilivyojaa ukweli wa Biblia ambao watu wanauhitaji.”
Shule Ya Sabato
Shule ya Sabato ambayo ni programu ya msingi ya elimu katika Kanisa, ina malengo manne:
kusoma maandiko, ushirika, huduma kwa jamii na kusisitiza utume ulimwenguni. Idara ya Shule ya Sabato na Huduma Binafsi ya Konferensi Kuu husambaza miongozo ya kusoma Biblia kwa viwango vyote vya umri, hutoa miundo ya programu za shule ya Sabato katika muktadha wa 105 utamaduni mbalimbali wa divisheni za ulimwengu, hutoa miongozo na mifumo ya mafunzo kwa ajili ya walimu wa shule ya Sabato, na huhamasisha utoaji wa sadaka za shule ya Sabato kwa ajili ya utume wa ulimwengu.
Huduma Binafsi
Huduma Binafsi hutoa zana na kufundisha washiriki kuunganisha ...
juhudi zao na zile za mchungaji na maofisa katika huduma ya kuongoa roho. Pia ina jukumu kubwa kwa ajili ya programu za kusaidia wahitaji.
Huduma Za Uwakili
Huduma za uwakili huhimiza washiriki kuitikia neema ya Mungu kwa kuweka wakfu kwake vyote walivyo navyo.
Majukumu ya uwakili ni zaidi ya pesa. Ni pamoja na utunzaji na utumiaji bora wa mwili, akili, muda, uwezo, karama za roho, na uhusiano, ushawishi, lugha, mazingira na mali. Idara hii husaidia washiriki katika ushirika wao na Mungu katika kumaliza kazi yake kwa kutumia vizuri karama na raslimali zote za Mungu. Roho wa Mungu anapotawala maisha ya mtu, “wale ambao mioyo yao imejaa upendo wa Kristo watafuata mfano wake ambaye alikuwa maskini kwa ajili yetu, ili kwa njia ya umaskini wake, tufanywe kuwa matajiri. Pesa, muda, ushawishi—karama zote walizopata kutoka mkononi mwa Mungu, watazithamini tu kama nyenzo za kuendeleza kazi ya injili.”
Huduma Za Wanawake
Huduma za wanawake huendeleza, huhimiza, na kuwapa changamoto wanawake katika kutembea kwao kila siku kama wanafunzi wa Yesu Kristo na washiriki wa kanisa lake.
Malengo yake ni kuhamasisha ukuaji wa kiroho na uamsho; kusisitiza kuwa wanawake wana thamani isiyopimika kwa sababu ya kuumbwa na kukombolewa kwao, kuwaandaa kwa ajili ya huduma na kueleza mitazamo ya wanawake katika masuala ya kanisa; 112 kuhudumia upeo wote wa mahitaji ya wanawake kwa kuzingatia mitazamo ya utamaduni na makabila mbalimbali; kushirikiana na idara zingine kurahisisha huduma za wanawake na kwa wanawake; kujenga mapenzi mema miongoni mwa wanawake,
Huduma Za Vijana
Vyama mbalimbali vya vijana kanisani havina budi kufanya kazi kwa karibu na idara ya huduma za vijana ya konferensi.
Chama cha Vijana wa Kiadventista (CVK)—Kanisa huhudumia vijana na kufanya nao kazi kwa kutumia CVK. Inawapasa vijana kufanya kazi pamoja chini ya kiongozi wa chama cha vijana katika kujenga huduma imara ya vijana inayojumuisha ustawi wa kila mmoja kiroho, kiakili na kimwili, shughuli za kijamii za Kikristo na programu hai ya ushuhudiaji inayosaidia mipango mikuu ya kanisa ya uongoaji wa roho. Lengo la chama cha vijana liwe kuwahusisha vijana wote katika shughuli zitakazowaunganisha na kanisa na kuwafundisha kwa ajili ya huduma ya Kikristo.
Muziki
Kuchagua Waratibu wa Muziki—Inalipasa kanisa kuwa na tahadhari kubwa katika kuchagua viongozi wa muziki, likichagua wale waliojitoa kikamilifu tu na kutoa muziki unaofaa kwa ajili ya huduma zote za ibada na mikutano. Muziki wa kidunia au ule uletao mashaka kwa namna ulivyo, usiingizwe katika ibada zetu.
Kuchagua Wapiga Muziki—Muziki mtakatifu ni sehemu muhimu ya ibada ya pamoja. Inalipasa kanisa kuwa na uangalifu katika kuchagua waimbaji na wapiga muziki wengine ambao watawakilisha vyema maadili ya Kanisa. Hawana budi kuwa washiriki wa kanisa, Shule ya Sabato, au Chama cha Vijana wa Kiadventista. Kwa kuwa wanashika nafasi inayoonekana katika ibada, inawapasa kuwa mfano wa staha na adabu katika kuonekana na mavazi yao. Majoho ya kwaya yanaweza kutumika.